HABARI MUHIMU KUELEKEA NORWICH vs CHELSEA - Darajani 1905

HABARI MUHIMU KUELEKEA NORWICH vs CHELSEA

Share This
Kuelekea mchezo wa kombe la FA hii leo ambapo Chelsea itasafiri mpaka jijini Norwich kumenyana na klabu ya jiji hilo yaani Norwich City FC, hapa nimekuletea mambo muhimu ya kuyafahamu katika mchezo huo ambao utachezwa usiku wa leo saa 08:30 usiku (saa 20:30) kwa saa za Afrika Mashariki katika uwanja wa klabu hiyo, Carrow Road.

Chelsea Habari muhimu: Chelsea imekuwa na wastani mzuri inapocheza na klabu ambayo haishiriki ligi kuu kama hii ya Norwich ambapo katika michezo 21 iliyokutana na klabu isiyoshiriki ligi kuu katika kombe hili la FA imefanikiwa kushinda michezo 20 huku ikipoteza mmoja. David Luiz atahusika katika mchezo huu kama inavyotarajiw mara baada ya kutoka majjeuhi aliyokuwa anayauguza yaliyomfanya kutoichezea Chelsea tangu mwezi Oktoba mwaka jana huku Charly Musonda naye kukiwa na uwezekano wa kuwemo mara baada ya kuwa nje akiuguza maumivu pamoja na Luiz.

 vs Norwich Habari muhimu: Kwa upande wa Norwich wao hawajapoteza katika michezo itatu iliyopita huku wakiongozwa vyema na Steven Naismith, aliwai kuichezea Everton na katika mchezo wa mwisho kuichezea Everton alitufunga magoli matatu huku jumla akiwa ameifunga Chelsea magoli 6.

Chelsea Majeruhi; Chelsea leo inaweza kucheza bila kuwa na Eden Hazard ambaye inaelezwa alipata majeraha katika mchezo dhidi ya Arsenal ulioisha kwa sale ya 2-2 wakati pia Baba Rahman naye pia atakosekana kutokana na majeruhi ya muda mrefu.

H2H: Mara ya mwisho kwa Chelsea kupoteza katika mchezo dhidi ya Norwich ilikuwa mwaka 1994 wakati huo mimi mwandishi hata sikuwepo duniani ambapo kipindi hicho Chelsea ilifungwa 3-0 lakini toka kipindi hicho, mpaka leo hii, Chelsea imecheza dhidi ya Norwich michezo 13 huku Chelsea ikishinda michezo 10 na kutoa suluhu michezo 3.

Mechi zilizopita;
Chelsea; WDWWD
 Norwich; LLWWW

Muda: Saa 08:30 Usiku (Saa 20:30)



No comments:

Post a Comment