ALICHOKISEMA BARKLEY BAADA YA KUTUA CHELSEA - Darajani 1905

ALICHOKISEMA BARKLEY BAADA YA KUTUA CHELSEA

Share This
Mara baada ya jana Chelsea kumtangaza rasmi nyota Ross Barkley kuwa mchezaji mpya wa Chelsea akisajiliwa akitokea klabu ya Everton au unaweza kuwaita The Toffes, nyota huyo hakuista kutoa neno mara baada ya kukamilishauhamisho huo.

Alipohojiwa alisema "Wakati nnakuwa nilikuwa nikiwatazama Frank Lampard na Michael Ballack kama nyota wangu, nao walishawai kuwa hapa (Chelsea). Haswa Frank Lampard nilikuwa nampenda sana. Nilijiona mwenye bahati sana nilipocheza na Frank timu ya taifa. Nilikuwa najifunza pia kutoka kwake tukiwa mazoezini, alikuwa ni mtu mwenye njaa ya magoli. Nami nimejifunza hilo kutoka kwake." alisema Barkley.

Mara baada ya kutambulishwa rasmi, nyota huyo alipewa jezi au fulana yenye namba 8 ambayo ilikuwa ikivaliwa na Frank Lampard na baadae Oscar Emboaba ambaye kwa sasa ametimkia nchini China akiwa anacheza soka huko toka mwezi januari mwaka 2017.

Lakini kwa upande wa Lampard mwenyewe ambaye ni gwiji wa Chelsea ambapo kwa sasa anafanya kazi kama mchambuzi wa soka, alipoulizwa kuhusu Barkley alijibu "Namfahamu Ross, ni mchezaji mwenye kipaji na ana uwezo pia. Nilifanya nae mazoezi tukiwa timu ya taifa na nilicheza dhidi yake kwenye ligi, nadhani ni kijana mzuri ukilinganisha pia na umri wake, nadhani anatazamia kufanikiwa na kwa kuwa yupo Chelsea basi nadhani aliowakuta pale watamfanya awe bora zaidi"

Je uamtazama Barkley kama mrithi halali wa Lampard?

No comments:

Post a Comment