KUMBE COURTOIS NI MUONGO, ANAITAKA MADRID - Darajani 1905

KUMBE COURTOIS NI MUONGO, ANAITAKA MADRID

Share This
Kuna taarifa kutoka kwa mwanahabari mmoja huko nchini Hispania ambaye amekuwa akifatiliwa sana kwa habari zake, Guillem Balague ambaye ametoa kauli kuhusu uhamisho wa kipa wa Chelsea, Thibaut Courtois kujiunga na Real Madrid ya nchini Hispania jijini Madrid.

Mwandishi huyo anasema haamini kwa kipa huyo raia wa Ubelgiji kwamba kusema kwake kuwa anakaribia kusaini mkataba mpya Chelsea ilikuwa ni taarifa ya kweli na badala yake kipa huyo alisema maneno hayo ili kuwafanya Real Madrid ifanye haraka kupeleka ofa kwa Chelsea ili imnase maana anachokitamani kwa sasa ni kwend jijini Madrid ambapo kuna familia yake ambayo aliipata akiwa klabuni Atletico Madrid ambapo alifika huko kwa mkopo na kupata familia ambayo mpaka leo ipo huko.

Thibaut Courtois amekuwa akifukuziwa na Real Madrid kwa muda mrefu huku akitazamiwa kwenda kuchukua nafasi ya kipa namba moja wa klabu hiyo, Keylor Navas ambaye anatazamiwa kuondoka klabuni hapo katika dirisha hili la usajili.

No comments:

Post a Comment