CHELSEA YABAKIZA KITU KIMOJA KUMNASA VIDAL - Darajani 1905

CHELSEA YABAKIZA KITU KIMOJA KUMNASA VIDAL

Share This
Kuna taarifa zinaeleza kuwa sasa Chelsea imebakiza kitu kmoja tu kuweza kumvuta kiungo raia wa Chile anayeichezea klabu ya Bayern Munich, Arturo Vidal ambapo taarifa hizo zinasema kilichobaki ili kumnasa nyota huyo ni Chelsea kukaa mezani na Bayern Munich na kukubaliana kiasi kinachotakiw kutolewa ili ununuzi wa nyota huyo ukamilike.

Taarifa hizo zinaeleza pia kuwa Chelsea imeshafanya makubaliano na nyota huyo huku kukiwa na makubaliano kwamba kama kiungo huyo akijiunga na Chelsea atapewa mkataba wa miaka minne na kupewa mshahara wa paundi milioni 13 kwa mwaka. Ambapo kwa hitaji hilo inaelezwa kwa nyota huyo amekubaliana lakini pia akionekana kuwa kipenzi cha kocha wa Chelsea, Antonio Conte ambaye walishawai kufanya kazi apmoja klabuni Juventus ambapo Conte alikuwa kocha kabla ya kujiunga na Chelsea.

No comments:

Post a Comment