KINDA MWENGINE WA CHELSEA KUTOLEWA KWA MKOPO - Darajani 1905

KINDA MWENGINE WA CHELSEA KUTOLEWA KWA MKOPO

Share This
Nyota na kinda wa Chelsea, Jake Clarke-Salter anaweza akaichezea Chelsea mchezo wake wa mwisho leo ambapo klabu hiyo itashuka uwanjani kumenyana na Norwich katika kombe la FA mara baada ya nyota huyo kutakiwa na klabu ya Sunderland ambayo anaweza kujiunga nayokwa mkopo katika dirisha hili dogo la usajili.

Salter aliichezea Chelsea mchezo wake wa kwanza mwaka 2016 mwezi Aprili huku akitumia muda mwingi akicheza kwa mkopo Bristol Rovers huku pia akiitumikia timu ya vijana ya Chelsea ambao ni chini ya miaka 23 huku mwenyewe akiwa na miaka 20 akiwa na uwezo mkubwa kucheza kama mlinzi wa kati huku akipata sifa kedekede kutoka kwa gwiji wa Chelsea, John Terry.

Hongera Clarke-Salter

No comments:

Post a Comment