Kumbe mama ndiye sababu ya Mbappe kushindwa kusajiliwa na Chelsea - Darajani 1905

Kumbe mama ndiye sababu ya Mbappe kushindwa kusajiliwa na Chelsea

Share This

Unakumbuka kuna moja ya picha zilizosambaa zikimuonyesha nyota wa klabu ya PSG na timu ya taifa ya Ufaransa, Kylian Mbappe zikimuonyesha akiwa na jezi ya Chelsea pindi alipokuwa bado.mdogo? unaikumbuka?

Sasa toka kuvuja au kusambaa kwa picha ile kulizua mzozo mkubwa na maswali mengi juu ya je nyota huyo aliwai kutua Chelsea? kwanini awe na jezi hiyo?
Kulitolewa majibu na baadhi ya watu kadhaa wengine wakisema kwamba Chelsea ilimpotezea na kuamua kuachana nae, lakini bado hakukupatikana jibu lenye ushahidi kamili.

Lakini leo nakuletea habari hii ambayo ina ukweli mkubwa kuhusu jambo hilo la mshindi huyo wa Kombe la Dunia kuwai kutakiwa na Chelsea.
Ilikuwa mwaka 2012 wakati moja ya maskauti au wasaka vipaji wa Chelsea, Serge Boga alipoitembelea nchi ya Ufaransa na huko alikutana na moja ya marafiki zake ambapo kwenye moja ya stori zao akasimuliwa kuhusu kijana huyo, Kylian Mbappe ambaye kwa kipindi iko alikuwa akicheza kwenye moja ya klabu za mtaani. Ndipo Boga akamwambia rafiki yake kwamba anataka akashuhudie kwa macho yake kipaji cha kinda huyo. Na kweli akaenda na akauona uwezo wa mtoto huyo.
Kylian Mbappe akiwa na baba yake

Akakutana na mzazi wa Mbappe kisha wakafanya mazungumzo.

Lakini kwa kuwa alikuwa ni skauti tu yaani msakata vipaji aliyeajiriwa na Chelsea akaamua kurejea jijini London ili kukutana na uongozi wa klabu hiyo, na moja ya mambo aliyowaambia ni kuhusu kipaji cha kinda huyo.

Basi kweli klabu ikaagiza kinda huyo asafirishwe kutoka nchini kwao Ufaransa mpaka nchini Uingereza akiwa sambamba na mama yake ambaye hakuwa akijua kuongea kiingereza.

Basi kinda huyo alipofika ikatakiwa ajaribiwe na ndipo akavaa jezi ya Chelsea na kucheza kwenye mchezo wa vijana wa akademi ambapo Chelsea iliondoka na ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Charlton katika uwanja wa mazoezi wa Chelsea.

"Mara baada ya kumuangalia tulifanya kikao nikiwa mimi, viongozi wa Chelsea pamoja na mama yake na Mbappe. Lakini mimi nilikuwa natumika pia kama mtafsiri kwa kuwa mama wa Mbappe alikuwa hajui kuzungumza kiingereza"

"Viongozi wa Chelsea wakaona walihitaji kumwangalia tena katika mchezo wa pili. Hivyo walisema ingekuwa vyema kama wakirudi tena siku kadhaa zinazofata ili wamwangalie tena katika mchezo mwengine"

"Lakini nilipomwambia mama yake akasema, hilo halitowezekana. Kama wanamchukua wamchukua sasa hivi, hiyo ya kusema tuje tena siku nyengine itakuwa ngumu. Huyu wanayemuona leo baada ya miaka mitano watamtaka kwa paundi milioni 50." alisema Boga alipokuwa akisimulia mkasa huo.

"Lakini mi nikamwambia hapana siwezi kuwaambia hivyo. Lakini ni kweli alichokisema"

"Lakini pia tatizo la Mbappe kipindi kile hakuwa mpambanaji. Kuanzia kwenye ukabaji hakuwa vizuri, nadhani hiyo ndiyo ilikuwa sababu walisema inatakiwa aje siku nyengine ili waone kama atabadilika." alisema Boga.

"Alikuwa anakokota mpira vizuri, lakini walihitaji kumuona anacheza vipi wakati akiwa hana mpira" alisema skauti huyo

Mbappe kwasasa ndiye mmoja wa wachezaji wenye thamani kubwa haswa kutokana na umri wake mdogo wa miaka 19 lakini tayari ameshafanya makubwa ikiwemo kuiongoza timu ya taifa ya Ufaransa kushinda michuano ya Kombe la Dunia huko nchini Urusi yaliyofanyika mwezi Juni mwaka huu na kumalizika mwezi Julai.

No comments:

Post a Comment