FIFA yatunga sheria ya kuitega Chelsea - Darajani 1905

FIFA yatunga sheria ya kuitega Chelsea

Share This
Kumekuwa na mabadiliko ya sheria yamekuwa yakiendelea kufanyika uku kanuni mpya zikiwa zikipendezwa ili zitumike katika michuano mbalimbali lakini haswa katika bara la Ulaya.

Mwishoni mwa mwezi uliopita kama sio mwanzoni mwa mwezi huu kuliripotiwa kwamba makocha wa klabu kadhaa wakiongozwa na aliyekuwa kocha wa zamani wa Chelsea ambaye kwasasa ni kocha wa klabu ya Manchester united, Jose Mourinho walipeleka maombi ya kufutwa kwa sheria ya ugenini ambayo imekuwa ikitumika katika michuano ya Ulaya ikiwemo michuano ya klabu bingwa barani Ulaya wakidai kwa miaka ya sasa hakuna ugumu kwa klabu iliyo ugenini kupata goli moja

Lakini pia ukiachana na hayo mengi yaliyotokea hapa karibuni ikiwemo klabu za Uingereza kupendekeza kubadilishwa kwa tarehe ya kufungwa kwa dirisha kubwa la usajili ambapo dirisha lililopita kwa nchini Uingereza lilifungwa tarehe 9-Agosti wakati katika nchi nyengine za barani Ulaya lilifungwa tarehe 31-Agosti.

Lakini hii leo kumetoka pendekezo jengine. Pendekezo jipya kutoka kwa chama cha soka duniani (FIFA) ambapo inaelezwa wamefikia maamuzi ya kubadilisha sheria ya wachezaji wa mkopo kutolewa kwa mkopo.

Sheria hiyo inaelezwa kwamba klabu yoyote itakuwa na ruhusa ya kutoa kwa mkopo wachezaji wasiozidi nane wenye mkataba kama wachezaji wa kulipwa ambao wana umri kuanzia miaka 21 wakati wale waliokuzwa na kuwa kama zao kuruhusiwa kucheza kwa mkopo.

Sheria hii imetungwa ili kuzizuia zile klabu zinazosajili wachezaji wengi uku ikiwatoa kwa mkopo na bila kuwatumia kwenye klabu zao.

Sheria hii inaonekana kuja vibaya kwa klabu ya Chelsea ambayo imekuwa ikiwatoa nyota wake wengi kwa mkopo uku kwasasa ikiwa na wachezaji 40 iliowatoa kwa mkopo.

No comments:

Post a Comment