CHELSEA YALETEWA SANDRO MLANGONI - Darajani 1905

CHELSEA YALETEWA SANDRO MLANGONI

Share This
Mara baada ya kuwepo kwa tetesi nyingi zikimhusisha nyota wa Juventus ambaye ni raia wa Brazil, Alex Sandro kuhusu kutakiwa na klabu nyingi barani Ulaya, kumbe zote ni tetesi na hakuna klabu yoyote iliyopeleka maombi kwa klabu ya nyota huyo ili imsajili.

Kioongozi mkubwa wa klabu hiyo ya jijini Turin nchini Italia, Giussepe Marota alipohojiwa juu ya hatma na tetesi za nyota huyo kutakiwa na vilabu vingi barani Ulaya haswa nchini Uingereza ambapo Chelsea imekuwa ikitajwa kwa karibu kumuwania nyota huyo, alisema "Kawaida ya Juventus, huwa pale mchezaji anapoufata uongozi na kuwaambia kuwa anahitaji kuondoka, huwa hakuna tatizo lakini pia hakuna klabu au mawasiliano yaliyofanyika ili kumtaka Sandro"

Kwa maneno ya kiongozi huyo inamaanisha Chelsea inaweza kupeleka maombi haraka kwa mchezaji huyo ili imsajili maana mpaka sasa hakuna klabu iliyopeleka ofa kwa klabu hiyo.

Unadhani Chelsea inamhitaji nyota huyu?

No comments:

Post a Comment