AKE WA CHELSEA AWASHA MOTO BOURNE - Darajani 1905

AKE WA CHELSEA AWASHA MOTO BOURNE

Share This
Unamkumbuka yule kinda aliyelelewa na Chelsea kabla ya kutolewa kwa mkopo klabuni,AFC Bournemouth ambapo baadae akauzwa kabisa? Anaitwa Nathan Ake, unamkumbuka vizuri? Alikuwa na rasta flani hivi, sasa huko alipo yaani Bournemouth amekuwa moto hatari, amekuwa mchezaji bora wa klabuni hapo kwa mwezi Desemba ambapo kwa mwezi huo amecheza michezo 7 huku akiukosa mchezo mmoja wa kombe la Carabao ambapo klabu yake ilimenyana na Chelsea na tuliwafunnga 2-1.

Nathan Ake ameshinda tunzo hiyo akishinda kwa kura 43% huku akiwabwaga nyota wenzake wa klabuni hapo ambao ni Ryan Fraser, Lewis Cook na Adam Smith.

Hongera Nathan Ake, nategemea siku utarudi Darajani 

No comments:

Post a Comment