HAZARD AKATAA TENA KUSAINI MKATABA MPYA - Darajani 1905

HAZARD AKATAA TENA KUSAINI MKATABA MPYA

Share This

Hii inakuwa kinyume na habari zilizosambaa katika magazeti mengi barani Ulaya, haswa nchini Uingereza zikidai nyota wa Chelsea, Eden Hazard huenda akasaini mkataba mpya akifatana na Thibaut Courtois, lakini pia zikisema Real Madrid imeachana na mpango wa kumsajili nyota huyo wa Chelsea.

Habari zilizopo kwa sasa zinazotoka kwa mwandishi wa habari mmoja maarufu, Mohamed Bouhafsi ni kuwa Eden Hazard amegoma tena kusaini mkataba mpya klabuni Chelsea huku sababu inayoelezwa ni kuwa nyota huyo anatazamia kujiunga na Real Madrid na sio kweli kwamba klabu hiyo imesitisha mpango wake.

Boufal anadai mara baada ya nyota huyo kukataa mara ya kwanza kusaini mkataba mpya, hii ni mara ya pili anagoma ambapo mkataba wake wa sasa unaisha 2022.

Taarifa hizo zinaendana na taarifa alizozitoa baba wa nyota huyo, Thierry Hazard ambaye naye alisema mtoto wake kutakiwa na Real Madrid kumemfanya asitishe kusaini mkataba mpya.

Hii ni habari mbaya kwa familia ya mashabiki wa Chelsea ambapo kila mmoja anaomba ziwe za uongo.

No comments:

Post a Comment