RASMI; BARKLEY NI MCHEZAJI WA CHELSEA - Darajani 1905

RASMI; BARKLEY NI MCHEZAJI WA CHELSEA

Share This

Hii ni habari rasmi kuwa kiungo raia wa Uingereza, Ross Barkley atakuwa ni mchezaji wa zamani wa Everton uku akiwa mchezaji mpya wa Chelsea.

Nyota huyo amekamilisha rasmi uhamisho wake wa kusajiliwa Darajani akitokea klabuni Everton, akisaini Chelsea kwa mkataba wa miaka mitano na nusu uku akikabidhiwa jezi yenye namba 8.

Barkley amekamilisha uhamisho huo mara baada ya kuhusishwa kwa muda mrefu kutua klabuni hapa na sasa matarajio ya wengi leo yamekamilika, ila ataanza kukaa nje kwanza kujiweka sawa mara baada ya kuwa na majeruhi.

Akihojiwa mara baada ya kutambulishwa, Barkley alisema "Ni furaha kuwa hapa na naamini nitatimiza mengi nikiwa na klabu mpya"

Karibu Ross Barkley

No comments:

Post a Comment