Ni kama tayari ashakuwa mchezaji wa Chelssea, kilichobaki kwa sasa ni kutangazwa rasmi tu kuwa mchezaji mpya wa Chelsea, huyo ni Ross Barkley ambaye dau lake la kutoka klabuni Everton na kutua Chelsea linatajwa kuwa paundi milioni 35. Kwa maana hiyo sasa kinachoangaliwa ni kuendelea na jitihada za nyota mwengin ili aongezwe klabuni Chelsea, na nyota huyo anayetajwa kukaribia katika mikono ya kocha Antonio Conte ni mchezaji bora wa liggi kuu Uingereza kwa msimu wa 2015-2016, mwarabu Riyad Mahrez.
Riyad Mahrez anatajwa kuhamishiwa nguvu mara baada ya kunaswa kwa Ross Barkley, amekuwa akihusishwa kwa muda mrefu sasa na mabingwa watetezi wa ligi kuu Uingereza, Chelsea lakini ikaaminika huenda kusajiliwa kwa Barkley kunaweza kukamfanya asitishe kuja lakini kwa fununu zilizokuwepo ni kuwa muda wowote majeshi yanaweza yakahamia kwa nyota huyo raia wa Algeria.
Kocha wake wa klabu ya Leicester, Claude Puel anaonekana kutotaka uvumi huo uendelee akisema ameshafanya mawasiliano na hata kukutana na nyota huyo lakini mara zote amekuwa akikiri kuwa ana furaha klabuni hapo.
Unadhani Chelsea itaendelea kumfukuzia winga huyo?
JE CHELSEA ITAENDELEA NA MAHREZ?
Share This
Tags
# Chelsea Usajili
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Usajili
Labels:
Chelsea Usajili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment