OWEN AMKATAA HAZARD - Darajani 1905

OWEN AMKATAA HAZARD

Share This
Nyota na gwiji wa soka wa zamani, Michael Owen ambaye aliwai kuzichezea klabu za Liverpumba na Manyumbu ameikataa penati iliyotokea katika mchezo wa Arsenyani ilipoikaribisa Chelsea juzi katika uwanja wa Emirates ambapo uliisha kwa suluhu ya 2-2.

Katika mchezo huo, Eden Hazard alichezewa madhami katika eneo la hatari akichezewa na mlinzi Bellerin ambapo mwamuzi wa mchezo aliamuru ipigwe penati na Hazrd akapiga mwenyewe kuifanya Chelsea ichomoe kutoka nyuma 1-0 mpaka kufanya mchezo kuwa 1-1 kabla ya baadae kidogo Marcos Alonso kufunga goli la pili na Bellerin kuchomoa katika dakika za nyiongeza.

Kutokana na penati hiyo iliyoibua mijadala mingi, mkongwe huyo amesema "Haikuwa penati, watu inabidi wajiulize je ni kweli mchezaji akiguswa katika eneo la hatari kisha akaanguka je ni penati? kugusana kunaruhusiwa kwenye mpira"

Lakini kwa kocha Antonio Conte alipoulizwa kuhusu penati hiyo alijibu "Arsene Wenger (Kocha wa Arsenyani) akiuangalia mchezo huo, atagundua likuwa na bahati sana kwa mwamuzi kutokuwa na maamuzi sahihi"

No comments:

Post a Comment