Chelsea iliwai kukamilisha usajili wa nyota wa kiarabu ambaye alisajiliwa akitoea klabu ya FC Basel, Mohammed Salah ambaye alitua Chelsea mwaka 2014 na kuondoka mwaka 2016 huku akitua hapo kwa dau la paundi milioni 11.
Nyota huyo hakuwa na mafanikio makubwa klabuni Chelsea licha ya kuhusika katika kikosi cha kocha Jose Mourinho kilichotwaa taji la ligi kuu Uingereza kwa msimu wa 2014-2015 na kikosi kilichotwaa taji la kombe la ligi kwa msimu huohuo. Ilikuwa ngumu kwake kumshawishi kocha wa Chelsea kwa kipindi iko, Jose Mourinho ambaye kwa sasa anaifundisha klabu ya Manyumbu (Man utd) ambapo muda mwingi aliutumia kuwa kwa mkopo kwenye vilabu kama vya Fiorentina na As Roma kabla ya baadae kuuzwa kwa jumla kujiunga na klabu hiyo ya As Roma kwa dau la euro milioni 15.
Gwiji wa soka wa Chelsea, Didier Drogba alipohojiwa juu ya maisha ya mchezaji huyo raia wa Misri alijibu "Kila mtu alikuwa naamini kuwa ni mchezaji mwenye kipaji na uwezo wa hali ya juu. Nadhani kwa sasa yupo chini ya kocha ambaye anampa majukumu makubwa na kumuamini. Hata ukimuangalia kwenye timu yake ya taifa anaaminika, na ndiye nyota mkubwa kwenye timu yao kwa sasa. Alipokuwa Italia (Fiorentina na As Roma) alionyesha kiwango kikubwa na sasa yupo Uingereza bado anaendeleza ubora wake. Ni mtu bora sana" alisema gwiji huyo ambaye ni mwafrika mwenzake.
Didier Drogba na Salah walikuwa pamoja wakati Chelsea inatwaa mataji hayo ya ligi kuu Uingereza lakini pia pamoja na kombe la ligi. Kocha Jose Mourinho amekuwa akipokea lawama nyigi juu ya kuvipoteza vipaji vya hali ya juu kuwai kutokea klabuni Chelsea na kwa sasa wanang'aa kwenye vilabu vingine.
Mohammed Salah kwa sasa ni mchezaji wa Liverpumba (Liverpool) na amekuwa mchezaji wa kutumainiwa katika klabu hiyo, lakinipia kuna mchezaji anaitwa Kevi de Bruyne ambaye mwenyewe hakuamaniwa kabisa na kocha Jose Mourinho na mpaka anaondoka Chelsea aliichezea michezo mitatu tu inayotambulia ukiachana na michezo ya kirafiki ambayo timu inachezakujiandaa na msimu mpya. Kwa kawaida ya Mourinho amekuwa sio mtu wa kuwaamini wachezaji vijana na kwa wakati huo De Bruyne alikuwa ndio kwanza ana miaka 20 licha ya kusaini kuichezea Chelsea kwa miaka mitano na nusu. Lakini kwa sasa nyota huyo ndiye anayechangia mafanikio kwa klabu ya Mama site (Man city) ambao kwa sasa ndio wapo kileleni mwa msimamo wa ligi kuu Uingereza.
DIDIER DROGBA ATOA NENO KUMHUSU ALIYEKUWA NYOTA WA CHELSEA
Share This
Tags
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment