Chelsea ilipata ushindi wake katika hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la Fa hapo jana dhidi ya Leicester na kufanikiwa kufudhu kucheza hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ambapo itacheza dhidi ya Southampton siku ya tarehe 21-Aprili huko jijini London kwenye uwanja wa taifa wa Uingereza maarufu kama Wembley, lakini kuna jambo lilitokea jana katika mchezo huo wa robo faianali pale King Power.
Ni tukio la nyota wa Chelsea, Willian Borges da Silva ambaye alionekana kutokuwa sawa kama mtu mwenye majeruhi licha ya kuchezewa vibaya na nyota wa klabu ya Leicester, ndipo kocha Antonio Conte akaamua kumtoa nyota huyo mara baada ya mchezo kuongezwa dakika 30, akimtoa muda mfupi mara baada ya dakika hizo kuongezwa na nafasi yake kuchukuliwa na Pedro Rodriguez aliyeifungia Chelsea goli la pili na la ushindi na kuisaidia Chelsea kufudhu kucheza hatua ya nusu fainali.
Kocha Antonio Conte alipoulizwa juu ya sababu ya nyota huyo kutolewa alisema "Willian alikuwa amechoka sana. Nadhani Willian ni mchezaji anayecheza vizuri akiwa na mpira na hata kama akiwa hana mpira. Ni mchezaji bora kwa hali zote na ninavutiwa na uwezo aliokuwa nao"
"Tuliamua kufanya uamuzi ule (wa kumfanyia mabadiliko) kwa kuwa alikuwa amechoka sana" na alipoulizwa juu ya kwanini aliamua kumtoa Andreas Christensen na nafasi yake kuchukuliwa na Gary Cahill, kocha huyo alitoa majibu kama alivyotoa kwa Willian kuwa wote walichoka.
"Walitumia nguvu kubwa kucheza dhidi ya Barcelona, na ilikuwa ngumu kwao kucheza dakika 120 dhidi ya Leicester maana walikuwa wamchoka sana na ukilinganisha na hali ya hewa ilivyo, isingekuwa rahisi kwao" alisema kocha huyo.
Lakini kwa upande wa Ross Barkley ambaye haonekani kuwa sawa kiafya na amekuwa nje kwa muda sasa akiuguza majeraha yake haionekani kama ataungana na kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza mara baada ya kocha wake kukiri nyota huyo amekosa nafasi ya kucheza kwa muda mrefu na ukilinganisha amekuwa majeruhi toka msimu uliopita, lakini kama atarejea kabla ya kumalizika kwa msimu mpya ambapo kama atapata nafasi ya kucheza na kuonyesha ubora basi anaweza akajumuishwa kwenye kikosi kitakachosafiri mpaka nchini Urusi na kujumuika na timu kwenye kombe la dunia.
Home
Chelsea FC
Chelsea Habari
ANTONIO CONTE AELEZA YA HALI YA WILLIAN, NA MWENGINE KUKOSA KOMBE LA DUNIA
ANTONIO CONTE AELEZA YA HALI YA WILLIAN, NA MWENGINE KUKOSA KOMBE LA DUNIA
Share This
Tags
# Chelsea FC
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea FC,
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment