Aliyekuwa mchezaji na kocha msaidizi wa Chelsea, Ray Wilkins kwa sasa anapigania uhai wake mara baada ya kukumbwa na ugonjwa wa mshtuko wa moyo ghafla na baadae kukimbizwa hospitali ya St. George ya jijini London. Nilikuletea taarifa hii, kama unataka kuisoma zaidi, bonyeza hapa.
Mara baada ya tukio hilo la kuskitisha, kocha wa Chelsea, Antonio Conte alitoa ujumbe wa kuonyesha kuhuzunishwa na taarifa hizo mbaya kwa mkongwe huyo ambaye kwa sasa ana miaka 61 kwa kusema "Kwanza nianze kwa kusema tupo karibu na Ray [Wilkins] pamoja na familia yake, lakini pia hata wachezaji naamini nao wapo nae karibu" alisema kocha huyo
Ray Wilkins alikuwa ni mchezaji klabu nyingi ingawa mojawapo ilikuwa klabu ya Chelsea lakini pia akiitumikia klabu hiyo kama mmoja ya makocha na watu muhimu kwenye benchi la ufundi la Chelsea.
No comments:
Post a Comment