Klabu ya akina dada ya Chelsea Ladies inatoka suluhu ya 1-1 ikiwa ugenini dhidi ya Arsenal Ladies katika mchezo wa ligi kuu Uingereza kwa wanawake au akinadada na kufanya kuongoza kwa tofauti ya alama tatu katika msimamo wa ligi kuu hiyo ya nchini Uingereza.
Nyota wa Chelsea, Fran Kirby ndiye alikuwa wa kwanza kuifanya Chelsea Ladies iliyochini ya kocha Emma Hayes, kocha wa zamani wa Arsenal kuwa mbele goli lililofungwa katika kipindi cha kwanza kabla ya goli hilo kusawazishwa na kufanya mchezo kwenda mapumziko huku matokeo yakiwa suluhu ya 1-1 dhidi ya klabu hiyo ya Arsenal iliyokuwa nyumbani.
Kipindi cha pili kilianza huku mashambulizi yakiwa ya kawaida huku Chelsea Ladies ikionekana kumiliki mpira na mchezo kwa kiasi kikubwa kuliko wapinzani wao, na hali ilitaka kuwa shwari kwa upande wa Chelsea mara baada ya nyota wake Cuthbert kupiga shuti kali kutoka umbali wa yard 15 lakini shuti hilo liliokolewa na mlinda mlango wa Arsenal Ladies.
Kwa matokeo hayo yanaifanya Chelsea Ladies kuendelea kuwa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu Uingereza kwa wanawake huku ikiwaacha kwa alama tatu wapinzani wake Manchester city inayoshika nafasi ya pili ingawa bado ina michezo miwili ambayo bado haijacheza.
No comments:
Post a Comment