Mlinda mlango nambari moja wa Chelsea, Thibaut Courtois jioni ya leo ameukosa mchezo mwengine dhidi ya Tottenham mara baada ya kuukosa mchezo uliopita dhidi ya Leicester kutokana na majeraha aliyoyapata akiwa mazoezini.
Kukosekana kwa nyota huyo raia wa Ubelgiji, kumewafanya waandishi wa habari kumuuliza kocha wa Chelsea, Antonio Conte juu ya kukosekana kwa mlinda mlango huyo mwenye miaka 25 kwa sasa.
"Courtois hajawa sawa kiafya. Na kwa hivyo inatulazimu tuwatumie wachezaji waliopo na waliokuwa tayari kucheza. Willy [Caballero] anacheza vizuri. Lakini pia Christensen nae amekuwa sawa" alisema kocha huyo akijibu swali hilo alipoulizwa juu ya nyota Courtois na Andreas Christensen.
Willy Caballero amekuwa akitumika kwa michezo yote ambayo Courtois ameshindwa kutumika lakini pia alichojibu juu ya Christensen ni kutokana na nyota huyo kukumbwa na majeraha yaliyomfanya kurudishwa kutoka kwenye kambi yake ya timu ya taifa ya Denmark ambapo kocha wake wa timu hiyo alikiri halitokuwa jambo sahihi kwa nyota huyo kuendelea kusalia na timu hiyo angali ana majeraha.
No comments:
Post a Comment