Chelsea inapoteza mchezo wake muhimu wa ligi kuu ikiwa nyumbani Stamford Bridge na kufanya mbio zake za kugombania nafasi nne za juu kuonekana kama zimekosa nguvu ambapo sasa imeachwa alama nane na Tottenham inayoshika nafasi ya nne huku Chelsea ikishika nafasi ya tano.
Goli la Chelsea lilifungwa na Alvaro Morata katika kipindi cha kwanza kabla ya mchezaji wa Tottenham kurudisha na kufanya mchezo kwenda mapumziko huku matokeo yakiwa 1-1.
Kipindi cha pili ndicho kilikuwa kibaya kwa Chelsea mara baada ya kushuhudia Chelsea ikiruhusu kufungwa magoli mawili yanayoifanya kupoteza mchezo wake muhimu kwenye ligi hiyo kuu nchini Uingereza.
Kilichoigharimu Chelsea ni udhaifu wake katika nafasi ya kiungo ambapo N'golo Kante na Cesc Fabregas walionekana kushindwa kabisa kuikabili safu ya kiungo na kuonekana kutawaliwa sana na mpira kumilikiwa na Tottenham kwa kiasi kikubwa.
Tottenham iliyoanza ikiwatumia zaidi viungo wake kama washambuliaji wakati wa kushambulia huku Harry Kane ambaye kiasili ni mshambuliaji wa kati hakuanzishwa kwenye mchezo huo, kuliifanya Chelsea kupitia kwa viungo wake Kante na Fabregas kuzidiwa na viungo wa Tottenham.
Kupoteza mchezo huo kwa Chelsea kunaifanya rekodi iliyodumu kwa miaka 28 kuvunjika ambapo Tottenham haikuwai kupata ushindi dhidi ya Chelsea kwenye uwanja wa Stamford Bridge. Mara ya mwisho kwa klabu hiyo kupata ushindi uwanjani hapo ilikuwa mwaka 1990.
No comments:
Post a Comment