Klabu ya Chelsea imeeleza kutoa mashtaka kwa chama cha soka barani Ulaya maarufu kama UEFA juu ya matukio ya kiunevu na udhalilishaji waliofanyiwa mashabiki wa klabu hiyo pindi klabu hiyo ya Chelsea iliposafiri na kwenda kumenyana na Barcelona kwenye mchezo wa klabu bingwa barani Ulaya, mchezo wa marudiano huko nchini Hispania.
Mara baada ya mchezo huo, kulisambaa video ikiwaonyesha mashabiki wa Chelsea wakifanyiwa udhalilishaji kwa kusukumwa na kutofanyiwa mpango mzuri wakati wa kutoka kwenye uwanja wa Barcelona mara baada ya mchezo kuisha, ambapo mchezo huo uliisha kwa Chelsea kupoteza kwa magoli 3-0 na kutupwa nje kwenye michuano hiyo katika hatua hiyo ya 16 bora.
Mara baada ya video hiyo kusambaa, klabu ya Chelsea ikatoa tangazo kwa wale mashabiki wa klabu hiyo waliokata tiketi maalumu kutoka kwenye klabu hiyo kutoa malalamiko yao huku wakiwa na ushahidi wa video au picha.
Muda wa kukusanywa malalamiko hayo ukatolewa na mashabiki waliokutwa na kadhia hiyo wakapeleka malalamiko yao na sasa uongozi wa klabu umetoa mrejesho kuwa tayari umeshapeleka malalamiko kwa uongozi wa chama cha soka barani Ulaya maarufu kama UEFA na inachosubiri kwa sasa ni majibu kutoka kwa chama hicho cha soka.
No comments:
Post a Comment