Kikosi cha timu ya klabu ya wanawake ya Chelsea maarufu kama Chelsea Ladies kimeshindwa kutetea nafasi yake ya kucheza fainali ya klabu bingwa barani Ulaya mara baada ya kupoteza mchezo wa nusu fainali usiku wa leo ikicheza dhidi ya Wolfburg kutoka nchini Ujerumani kwa magoli 2-0.
Chelsea Ladies ambayo ilisafiri hapo jana na kufanikiwa kufika nchini humo kucheza mchezo huo wa nusu fainali imeshindwa kufudhu katika hatua hiyo ya nusu fainali kutokana na kupoteza kwa matokeo ya jumla ya magoli 5-1 ambapo mchezo wa kwanza ambao Chelsea Ladies ilikuwa nyumbani ilipoteza kwa magoli 1-3 huku nyota wa Chelsea, Ji So-Yun akifunga goli pekee la Chelsea Ladies.
Sasa klabu hiyo ya Wolfburg Ladies itacheza mchezo wa fainali siku ya tarehe 24-May huku Chelsea Ladies ikijiandaa na msimu ujao.
No comments:
Post a Comment