Wanahitaji ushindi katika mchezo dhidi ya Deportivo ili kujitangaza kuwa mabingwa wapya wa michuano ya ligi kuu nchini Uingereza. Ni klabu ya Barcelona ya nchini humo, lakini kutolewa kwao katika hatua ya robo fainali ya klabu bingwa barani Ulaya kunatajwa kuwavuruga akili na sasa wanapanga kufanya usajili mkubwa katika dirisha kubwa la usajili. Wachezaji wanne wanatajwa kuingia kwenye mipango ya klabu hiyo ili kujiweka sawa kwa ajili ya msimu ujao.
Gazeti la nchini Hispania maarufu kama Don Balon limeripoti kuwa kati ya majina hayo manne yanayotajwa na klabu hiyo, kuna jina moja la mchezaji kutoka Chelsea.
Naye sie mwengine, ni Marcos Alonso anayecheza nafasi ya ulinzi wa kushoto huku akisifika kwa uwezo wake mkubwa wa kuhusika kwenye ushambuliaji huku mpaka sasa akiwa ameshaifungia Chelsea magoli sita kwa msimu huu anatajwa kwa karibu na klabu hiyo ya nchini Hispania ambako huko aliwai kuichezea klabu ya Real Madrid kwamba inawania saini yake ili kujiimarisha vyema kupambania taji la klabu bingwa barani Ulaya kwa mwaka 2019.
No comments:
Post a Comment