Mount wa Chelsea ashinda tunzo ya uchezaji bora - Darajani 1905

Mount wa Chelsea ashinda tunzo ya uchezaji bora

Share This

Ana miaka 19 kwa sasa na tayari ameshaichezea klabu ya Vitesse michezo 25 huku akiifungia magoli 9 na kutengeneza mengine 8 na amekuwa msingi na muhimili mkubwa kwenye kikosi hicho cha Vitesse ambacho anakichezea kwa mkopo, nyota huyo kutoka Chelsea, Mason Mount amefanikiwa kushinda tunzo ya mchezaji bora wa mwaka kwa upande wa mashabiki.

Klabu hiyo ya Vittese ilitangaza kupitia mtandao wa Twitter kuwa nyota huyo amefanikiwa kuchaguliwa kuwa mshindi wa tunzo hiyo aliyochaguliwa na mashabiki wa klabu hiyo kutokana na uwezo na mchango mkubwa aliouonyesha katika klabu hiyo anayoichezea kwa mkopo.

Mount anakuwa mchezaji wa tatu kutoka Chelsea kushinda tunzo hiyo katika klabu hiyo ambapo waliomtangulia ni pamoja na Christian Atsu aliyeshinda tunzo hiyo msimu wa 2013-2014 na Slobodan Rajkovic aliyeshinda msimu wa 2010-2011.

No comments:

Post a Comment