Kurt Zouma achaguliwa mchezaji bora - Darajani 1905

Kurt Zouma achaguliwa mchezaji bora

Share This

Nyota wa Chelsea, Kurt Zouma anayeichezea klabu ya Stoke city aliibuka kuwa mchezaji bora wa mchezo wa ligi kuu Uingereza ambapo klabu hiyo ilimenyana dhidi ya Liverpool na kuisha kwa sare ya 0-0.

Nyota huyo raia wa Ufaransa aliibuka nyota katika mchezo huo na kuutumia mtandao wa Twitter kutuma ujumbe ili kuonyesha furaha yake ya kuibuka nyota wa mchezo huo lakini pia akisema hiyo haitomaanisha kusimamisha mapambano na badala yake akawahasa wachezaji wenzake kuwa waendelee kupambana katika michezo iliyobaki ili kujiweka kwenye nafasi nzuri na kuepuka kutokushuka daraja.

Nakukumbusha kitu linalomhusu mlinzi huyu aliyesajiliwa na Chelsea akitokea St. Etienne, mchezaji raia wa Uingereza, Peter Crouch aliwai kutoa sifa juu ya mlinzi huyu akimsifia juu ya uwezo wake mkubwa na anavyopambana kuitetea klabu hiyo lakini jambo kubwa alilisema wachezaji wengine waliopo kwa mkopo kwenye klabu fulani ambayo haina msimu mzuri huwa wanajitenga na kukaa pembeni, hawapambani kwa ajili ya timu ambapo hiyo ni tofauti na alivyo Kurt Zouma ambaye anapambana kwa nguvu zote licha ya klabu hiyo kuwa katika nafasi ya hatari ya kushuka daraja.

Je unadhani anastahili kurejea kwenye kikosi cha Chelsea kwa msimu ujao?

No comments:

Post a Comment