Gwiji wa Chelsea amfananisha Loftus-Cheek na Mohammed Salah - Darajani 1905

Gwiji wa Chelsea amfananisha Loftus-Cheek na Mohammed Salah

Share This

Gwiji wa Chelsea, Tony Cascarino raia wa Jamhuri ya Ireland ambaye aliwai kuichezea Chelsea katika nafasi ya ushambuliaji ameitahadharisha klabu yake hiyo ya zamani juu ya kiungo wake anayeichezea klabu ya Crystal Palace kwa mkopo akisema ni lazima Chelsea imtumie nyota huyo katika kikosi chake cha msimu ujao kama haitaki kushuhudia kikiwatokea kama kilichowatokea kwa kumdharau Mohammed Salah ambaye kwa sasa anatamba klabuni Liverpool huku akichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa ligi kuu nchini Uingereza.

"Chelsea inatakiwa isikubali kwa fungu lolote la pesa kwa kumuacha Loftus-Cheek ili ajiunge na klabu nyengine. Ni lazima imjumuishe kwenye klabu hiyo kwa msimu ujao na impe muda zaidi wa kucheza." alisema gwiji huyo ambaye kwa sasa anafanya kazi ya uchambuzi.

"Ana uwezo mkubwa kutengeneza magoli na hata mwenyewe kuhusika kwenye ufungaji. Kamwe isimruhusu kuondoka kama alivyoondoka Mohammed Salah na De Bruyne maana naamini akitimiza miaka 22 kwenye klabu nyengine tayari atakuwa kiungo bora zaidi. Naamini kwa uwezo aliounyesha atakuwa mtu sahihi kwenye safu ya kiungo ya msimu ujao" aliendelea kusema.

Gwiji huyo amemfananisha Cheek na Mohammed Salah pamoja na De Bruyne ambao walisajiliwa na Chelsea lakini hawakupewa nafasi ya kucheza na hivyo kuishia kuuzwa ingawa kwa sasa ndio wanaotajwa kuwa wachezaji bora kwenye ligi kuu Uingereza.

Loftus-Cheek aliifungia Crystal Palace goli lake la kwanza tangu arejee kutoka kwenye majeraha, goli hilo alilifunga katika mchezo wa juzi ambapo Crystal iliitandika Leicester magoli 5-0 huku Cheek akihusika kwenye ufungaji na huenda akawa na nafasi ya kucheza kombe la dunia litakaloanza mwezi Juni mwaka huu mara baada ya nyota mwenzake anayecheza nafasi zinazofanana, Oxlade Chamberlain kupata majeraha yatakayomweka nje kwa muda mrefu na kulikosa kombe hilo.

No comments:

Post a Comment