Chelsea inatajwa kuandaa dau la paundi milioni 45 ili kumsajili nyota raia wa Ubelgiji anayeichezea klabu ya Tottenham, Toby Alderwield ambaye pia anatakiwa na klabu ya Manchester united.
Chelsea inatajwa kumfukuzia mlinzi huyo mwenye miaka 29 ambaye inaonekana amepoteza nafasi kwenye kikosi cha kwanza tangu klabu hiyo imsajili mlinzi raia wa Colombia, Davinson Sanchez ambaye kwa pamoja na Vertonghen wanaonekana kuimarika katika safu ya ulinzi ya klabu hiyo.
Lakini pia wakati huohuo, gazeti la The Sun limeendelea kuripoti kuwa Chelsea inamfukuzia kocha wa klabu ya Tottenham, Mauricio Pochettino ambaye ameiongoza vyema klabu hiyo ya Tottenham ili arithi nafasi ya kocha wa sasa klabuni The Blues, Antonio Conte ambaye amekuwa akitajwa kuwa na maisha mafupi ya kusalia klabuni hapo.
No comments:
Post a Comment