Chelsea yatwaa ubingwa wa kombe la FA - Darajani 1905

Chelsea yatwaa ubingwa wa kombe la FA

Share This

Klabu ya vijana ya Chelsea maalumu kwa vijana wenye umri chini ya miaka 18 maarufu kama Chelsea U18s wamefanikiwa kushinda na kutwaa taji la kombe la FA mara baada ya kuibamiza klabu ya vijana ya Arsenal U18s inayofundishwa na kocha Kwame Ampadu ambaye ni baba mzazi wa mchezaji wa Chelsea, Ethan Ampadu ambaye kwa sasa anauguza majeraha.

Chelsea ilishuka kwenye mchezo wa leo huku ikiwa na faida ya kupata ushindi kwenye mchezo wa kwanza wa fainali hizo ambapo kwa kawaida huwa inachezwa michezo miwili nyumbani na ugenini na bingwa au mshindi hupatikana kwa matokeo ya jumla na mchezo wa kwanza ulichezwa Stamford Bridge ambapo Chelsea U18s ilifanikiwa kupindua matokeo toka 0-1 mpaka kupata ushindi wa mabao 3-1 ilihitaji kupata ushindi wowote au ipate suluhu kwenye mchezo wa leo ili iweze kulitwaa taji hilo la kombe la FA ambapo Chelsea ndio mabingwa watetezi wakiwa wamelibeba taji hilo mara nne mfululizo.

Goli la mapema la Gilmour liliifanya Chelsea kuongoza katika fainali hii ya marudiano, ambapo goli hilo likifungwa dakika ya 11 na kuifanya Chelsea imalize kipindi cha kwanza ikiongoza kwa goli hilo 0-1 na kufanya matokeo ya jumla kuwa Arsenal 1-4 Chelsea.

Kipindi cha pili kilianza, na ikamuhitaji dakika 12 tu ili aifungie Chelsea goli la pili katika mchezo huo, huyo ni Hudson-Odoi ambaye alifunga goli hilo dakika ya 57. Anjorin akaifungia tena Chelsea goli la tatu katika dakika ya 67 na Hudson-Odoi kuifungia tena Chelsea goli la nne na kukamilisha ushindi wa magoli 0-4 huku ushindi wa jumla ukiwa Arsenal 1-7 Chelsea.

Kwa matokeo hayo, Chelsea inafanikiwa kulitwaa taji hilo la kombe la FA ikiwa ndio timu pekee kwenye ngazi ya vijana kuwai kulitwaa taji hilo mara ya tano mfululizo.

Hongereni vijana..

No comments:

Post a Comment