Kocha wa vijana ampa ushauri Antonio Conte kuhusu Hudson-Odoi - Darajani 1905

Kocha wa vijana ampa ushauri Antonio Conte kuhusu Hudson-Odoi

Share This

Achana na ubora aliouonyesha kwenye mchezo wa marudiano ya kombe la FA katika uwanja wa Emirates hii leo, ambapo Chelsea ilifanikiwa kuondoka na ushindi wa magoli 0-4 ikiwa ugenini dhidi ya Arsenal na kufanikiwa kutwaa taji hilo la vijana chini ya miaka 18 ya kombe la FA huku nyota huyo akiifungia Chelsea magoli mawili katika ushindi huo wa magoli manne huku ikishinda kwa jumla ya magoli 1-7.

Ni Callum Hudson-Odoi, kijana machachari anayeiongoza vyema klabu hiyo ya vijana huku pia ikifanikiwa kufanya makubwa msimu huu huku nyota huyo mwenye miaka 17 akiwa muhimili mkubwa kwenye kikosi hicho kilichochini ya kocha Jody Morris.

Kocha huyo, ametoa neno kuhusu alivyo nyota wake huyo, akisema "Tunatakiwa kuona na kusubiri, kocha mkuu (Antonio Conte) ataamua lipi kulifanya maana kwa sasa akiifikiria sana kikosi cha wakubwa. Sidhani kama akiwa peke yake ataweza kuyatimiza majukumu yote mwenyewe"

"Ana kazi kubwa ya kupambana na kujitahidi kuwa mchezaji aliyekamilika. Atakutana na mengi makubwa yatakayomfanya akate tamaa lakini bila shaka ataendelea kuwa bora maana ashalionyesha hilo. Ameonyesha kuimarika na kupevuka ila kikubwa anahitaji kupata maelekezo"

"Ana mambo mengi atakayotakiwa kujifunza na kuyaweka sawa na anatakiwa atambue ana mengi ya kujifunza na kuyaweka sawa kama mchezaji maana uwanjani kuna wachezaji wengi." alisema kocha huyo akimuhusia Hudson-Odoi kuhusu maisha yake ya kisoka lakini pia akimtetea kocha wa kikosi cha wakubwa kuwa bado anahitaji atulie ili aweze kukitumia vyema kipaji cha nyota huyo raia wa Uingereza.

No comments:

Post a Comment