Sarri, Antonio Conte wapishana kiamani - Darajani 1905

Sarri, Antonio Conte wapishana kiamani

Share This

Chombo cha habari cha nchini Italia ambacho kinadhaminiwa na klabu ya Napoli kimetoa taarifa ya kushtusha kidogo ambapo kimeripoti kuwa klabu hiyo ya Napoli inajiandaa kufanya mabadilishano na klabu ya Chelsea kwa upande wa benchi la ufundi.

Ripoti hiyo inadai kuwa klabu ya Napoli ipo tayari kumruhusu kocha wake, Maurizio Sarri akaondoka klabuni hapo huku majina yanayotajwa kuwaniwa na klabu ili kumrithi Sarri likitajwa pia jina la kocha wa Chelsea, Antonio Conte.

Taarifa zinadai rais wa klabu hiyo ya Napoli ameshindwa kufikia makubaliano binafsi na kocha huyo maarufu kwa kuvuta sigara akiwa uwanjani ambaye amekuwa akitajwa kutamaniwa na mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich kuwa atue klabuni hapo na dau linalotakiwa litolewe ili kumnasa likiwa ni paundi milioni 8 na inaelezwa Chelsea ipo tayari kutoa dau hilo ili kumnasa wakati huohuo jina la kocha Antonio Conte likatajwa kuwaniwa na klabu hiyo akitokea Chelsea.

No comments:

Post a Comment