Klabu ya Napoli ya nchini Italia inaripotiwa kuingia kwenye mpango wa kumsajili mlinzi kutoka nchini Brazil anayeichezea Chelsea, David Luiz kwenye majira ya dirisha la usajili la kipindi cha kiangazi linalofunguliwa mara baada ya msimu wa ligi kuu kumalizika.
Klabu hiyo inayofundishwa na kocha anayetakiwa na Chelsea, Maurizio Sarri inatajwa kuiwania saini ya mlinzi huyo mwenye miaka 31 kwa sasa huku ikiaminika usajili huo unaweza kukamilika ikitegemeana na mipango ya klabu ya Chelsea juu ya kocha wake Antonio Conte kama ataendelea kusalia klabuni hapo au laah. Vyanzo kadhaa vimekuwa vikiripoti mahusiano mabaya yaliyopo kati ya mlinzi huyo na kocha huyo ambapo inadaiwa mustakabali wa mlinzi huyo kusalia klabuni hapo utajulikana endapo Chelsea itaachana na kocha huyo raia wa Italia.
Lakini pia Darajani 1905 inaamini Napoli inamtaka David Luiz ili kuziba pengo la mlinzi wake, Kalidou Koulibaly anayetajwa kuwaniwa kwa karibu na Chelsea na kama Chelsea itahitaji impate Koulibaly basi italazimika pia imuache David Luiz ajiunge na klabu hiyo ya nchini Italia ingawa pia Darajani 1905 inaamini kocha Antonio Conte ndiye anayeshawishi usajili wa Koulibaly kutua Chelsea na kama akifanikiwa kutua klabuni hapo itakuwa tiketi kwa Luiz ili aondoke maana itamaanisha pia kwa Antonio Conte kuendelea kuwa kocha wa Chelsea. Na ndio hapo Napoli inapopata nguvu ya kumnasa.
No comments:
Post a Comment