David Luiz amekuwa hatumiki tena kama msimu uliopita ndani ya klabu ya Chelsea ikiwa chini ya kocha Antonio Conte ambaye anadai sababu ya nyota huyo raia wa Brazil kutokucheza ni majeraha aliyoyapata toka msimu ulioisha ingawa alimudu kucheza na kumaliza msimu mzima huku akiendelea kuwa mlinzi imara katika safu ya ulinzi ya Chelsea.
Ilielezwa hayupo kwenye hali nzuri tangu katika mchezo wa klabu bingwa Ulaya ambapo Chelsea ilikuwa ugenini dhidi ya As Roma ingawa alifanikiwa kurudi tena uwanjani katika mchezo wa ligi kuu Uingereza ambapo Chelsea ilipoteza mbele ya Watford na toka kipindi iko amekuwa mtu wa kutoshiriki hata kwa wachezaji wa akiba na kocha Antonio Conte akisema kukosekana kwa nyota huyo ni kutokana na majeraha.
Kutokana na hali hiyo klabu kadhaa zimekuwa zikitajwa kutamani kuipata huduma ya mlinzi huyo ambaye anaonekana kutamani kusalia Chelsea na ikiendelea kuripotiwa kuwa nyota huyo ataendelea kusalia Chelsea endapo kocha Antonio Conte ataondoka klabuni hapo. Tayari klabu ya As Monaco inatajwa kupeleka maombi ya kumsajili mlinzi huyo.
Kocha Antonio Conte aliwai kuulizwa juu ya nyota huyo kurejea uwanjani alisema hajui lolote kuhusu nyota huyo na bado hajajua kama ni muda gani atarejea uwanjani.
Lakini pia ukiachana na hayo yote, nyota huyo alifanya sherehe ya kumbukumbu yake ya kuzaliwa ya miaka 31 lakini kioja kikaibuliwa kwa kocha wake huyo kutokuonekana kwenye sherehe hizo ambapo ilidaiwa kuwa hakupewa mwaliko kutoka kwa mlinzi huyo na badala yake ukaudhuriwa na wachezaji wenzake wa Chelsea na baadhi ya marafiki zake na watu wa karibu.
No comments:
Post a Comment