Chelsea inafanikiwa kupata ushindi wa bao 0-1 dhidi ya Swansea pale Liberty Stadium na kufanikiwa kufikisha alama 66 kwenye msimamo wa ligi kuu Uingereza, bao hilo pekee lilifungwa na nyota raia wa Hispania, Cesc Fabregas.
Lakini je wajua kuna rekodi zimetengenezwa katika ushindi huo muhimu kwa Chelsea? mfungaji wa goli hilo ambaye ni Cesc Fabregas amefanikiwa kuweka rekodi mpya ya kuwa mhispania watatu kufikisha magoli 50 katika ligi kuu ya Uingereza akitanguliwa na wahispania wenzake ambao ni Fernando Torres pamoja na Diego Costa ambao wote walipita klabuni Chelsea.
Ukiachana na Fabregas, kocha Antonio Conte nae amefanikiwa kuweka rekodi mpya ya kupata ushindi kwa haraka kwenye michezo 50 ya ligi kuu Uingereza huku akiachwa na makocha wawili katika kuifikia rekodi hiyo ambao ni Jose Mourinho ambaye ameshinda michezo 50 katika michezo 63 wakati Pep Guardiola aliifika rekodi hiyo kwa kucheza michezo 69 wakati Conte katika michezo 73.
No comments:
Post a Comment