Klabu ya vijana wenye umri chini ya miaka 19, Chelsea U19s imeshindwa kupata ushindi katika mchezo wa leo ambapo ilikuwa inacheza fainali ya klabu bingwa barani Ulaya kwa soka la vijana (UYL) dhidi ya Barcelona mara baada ya kupoteza kwa mabao 0-3, mchezo ukichezwa uko jijini Nyon nchini Switzerland.
Chelsea ilishuka uwanjani ikiwakosa nyota wake Trevoh Chalobah mwenye adhabu ya kukosa mchezo lakini pia ikimkosa Ethan Ampadu aliyekuwa na majeraha na ikaanza mchezo uku ikiruhusu kufungwa goli moja katika kipindi cha kwanza na kipindi cha pili ikiruhusu magoli mawili na hivyo kushindwa kulitwaa taji hilo la barani Ulaya.
Chelsea na hata hapo ilipofikia imefanikiwa kuonyesha kwa kiasi gani ina hadhina kubwa ya vipaji kwa kufanikiwa kufikia fainali ya tatu ndani ya misimu minne mfululizo.
No comments:
Post a Comment