Chelsea imefanikiwa kufudhu kucheza hatua ya fainali ya kombe la FA mara baada ya kupata ushindi mnono wa magoli 2-0 dhidi ya Southampton hapo jana katika mchezo wa nusu fainali.
Kupata kwa Chelsea ushindi katika mchezo huo kulimuacha kocha wa Southampton, Mark Hughes akiwa na malalamiko juu ya maamuzi yaliyofanywa na mwamuzi wa mchezo huo Martin Atkinson tukio lililomfanya aingie kwenye malalamiko ni pale mlinda mlango wa Chelsea, Willy Caballero alipojaribu kudaka mpira huku akiwa sambamba na mshambuliaji wa Southampton, Charlie Austin kwenye eneo ls boksi dogo na mpira kumporonyoka mlinda mlango na kuingia golini kabla ya kipa huyo kuuwai. Tukio hilo lilitolewa maamuzi kuwa ilitakiwa upigwe mpira wa adhabu kuelekea upande wa Southampton ikidaiw Austin alimchezea madhambi mlinda mlango.
Baada ya mchezo huo kocha wa Southampton alitoa malalamishi akidai ile lilikuwa ni goli halali, wakati kocha huyo aliyewai kuwa mchezaji wa Chelsea akisema hivyo, mchambuzi mwengine wa soka kwenye chombo cha habari cha BT Sport, Frank Lampard amesema Southampton wamenyimwa haki na walifunga goli halali huku akidai hakuna makosa yaliyofanyika maana hakuna sheria inayosema kipa hatakiwi kuguswa kama alivyoguswa Caballero kwenye mchezo huo.
Lakini chama cha soka cha Uingereza ambacho kinasimamia soka nchini humo kimedai haikuwa na haja ya mwamuzi Atkinson kutumia teknolojia ya video maarufu kama VAR haswa kutokana na mwamuzi huyo kuwa na uhakika na tukio hilo na maamuzi aliyoyatoa na hivyo kupingana na Lampard aliyedai Southampton imeonewa.
No comments:
Post a Comment