Nyota wa Chelsea aibuka mchezaji bora wa Uingereza - Darajani 1905

Nyota wa Chelsea aibuka mchezaji bora wa Uingereza

Share This

Klabu ya soka ya wanawake ya Chelsea maarufu kama Chelsea Ladies imefanikiwa kumtoa mchezaji aliyefanikiwa kutwaa tunzo ya mchezaji bora wa mwaka katika ligi kuu Uingereza. Fran Kirby anayecheza nafasi ya ushambuliaji amefanikiwa kushinda tunzo hiyo inayotolewa na chama cha wanasoka wakulipwa maarufu kama PFA Player of the year.

Nyota huyo ameiongoza vyema Chelsea Ladies kufika mafanikio msimu huu huku ikifukuzana na Manchester city katika kugombania ubingwa wa ligi kuu Uingereza ambapo nyota huyo ameshaifungia Chelsea Ladies magoli 22, hiyo ikiwa ni kwa msimu huu tu kwenye michuano yote.

Fran Kirby pia alifanikiwa kuingia kwenye kikosi bora cha mwaka au cha msimu akiungana na nyota wengine watano kwenye kikosi hicho, wachezaji wa Chelsea Ladies ni Millie Bright, Ji So-Yun, Maren Mjelde na Hannah Blendell pamoja na Kirby mwenyewe.

No comments:

Post a Comment