Chelsea kupandisha mlima ugenini? - Darajani 1905

Chelsea kupandisha mlima ugenini?

Share This

Jana ilikuwa siku mbaya kwa kikosi cha wakinadada cha Chelsea Ladies mara baada ya kukosa kupata ushindi katika mchezo wake wa klabu bingwa barani Ulaya ambapo ilipoteza kwa magoli 1-3 dhidi ya Wolfburg na kujitengenezea mazingira magumu katika mchezo wa marudiano wa nusu fainali hiyo ya klabu bingwa.

Chelsea Ladies iliyokuwa nyumbani ilianza kupata goli la mapema kupitia kwa nyota wake Ji So-Yun na kuifanya Chelsea Ladies kuanza vizuri, lakini tabu ikaanza mara baada ya wapinzani kulishambulia lango la Chelsea na hatimaye wakafanikiwa kupata ushindi huo unaowapa kujiamini kuvuka hatua hiyo.

Kutokana na matokeo hayo ya 1-3, Chelsea Ladies ili ifudhu basi inatakiwa ipate ushindi wa kuanzia mabao 3-0, au ianzie manne na kuendelea lakini apate magoli mengi ugenini. Au unaweza kusema apate ushindi wenye tofauti ya magoli matatu na kuendelea. Lakini kama akishinda 3-1 kwenye mchezo unaofata basi itaangaliwa kama ziongezwe dakika thelathini au zipigwe penati. Mchezo wa marudiano utachezwa tarehe 29-Aprili.

No comments:

Post a Comment