Kikosi cha vijana wa umri chini ya miaka 19 cha Chelsea, maarufu kama Chelsea U19s kitashuka uwanjani jioni ya leo kucheza mchezo wake wa fainali ya ligi kuu Uingereza kwa vijana wa chini ya miaka hiyo ambapo itacheza mchezo huo dhidi ya Barcelona.
Chelsea U19s wamefikia hatua hiyo ya fainali mara baada ya kuondoka na ushindi wa matuta siku ya ijumaa ilipoifunga mabao 5-4 katika matuta klabu ya vijana ya FC Porto ambapo muda wa kawaida wa mchezo uliisha kwa sare ya 2-2, na shukrani zitapelekwa kwa goli la jioni la Josh Grant aliposawazisha na kufanya mchezo huo kuisha kwa sare hiyo ya magoli 2-2 lakini pia shukrani zimwendee mlinda mlango Cumming aliyeokoa penati tatu katika hatua hiyo ya matuta na hatimaye Chelsea ikafudhu kwa sare ya 2-2.
Chelsea itacheza fainali yake hiyo dhidi ya Barcelona muda wa saa 07:00 Usiku (Saa 19:00) kwa saa za Afrika Mashariki.
No comments:
Post a Comment