Conte atoa neno kucheza fainali dhidi ya 'Little Man' Mourinho - Darajani 1905

Conte atoa neno kucheza fainali dhidi ya 'Little Man' Mourinho

Share This

Chelsea imefanikiwa kufudhu kucheza fainali ya kombe la FA ambapo itacheza dhidi ya Manchester united kwenye uwanja wa Wembley uliopo jijini London nchini Uingereza. Kuelekea kwenye mchezo huo unaowakatunisha makocha waliowai kuingia kwenye vita ya maneno hapo awali kocha wa Chelsea, Antonio Conte na kocha wa Man utd, Jose Mourinho ambaye alishawai kuifundisha Chelsea, kocha Antonio Conte ametoa neno kuelekea kwenye mchezo huo na jinsi gani amejipanga kumenyana na mpinzani wake huyo raia wa Ureno.

"Kiukweli tofauti iliyopo kati yangu nayeye tulishaimaliza, tupo sawa. Hakika utakuwa ni mchezo wa klabu mbili kubwa" alisema kocha Antonio Conte ambaye mara ya mwisho wakiwa kwenye vita ya maneno alimuita Mourinho kuwa ni bwana mdogo 'little man'.

Mpaka sasa Antonio Conte ameiongoza Chelsea kucheza dhidi ya Man utd ya kocha Jose Mourinho kwenye michezo 5 ya michuano yote huku kocha Antonio Conte akifanikiwa kupata ushindi katika michezo mitatu na kupoteza michezo miwili.

No comments:

Post a Comment