'See you at Wembley', Chelsea dhidi ya Man utd fainali kombe la FA - Darajani 1905

'See you at Wembley', Chelsea dhidi ya Man utd fainali kombe la FA

Share This

Chelsea inafanikiwa kufika fainali ya kombe la FA mara mbili ndani ya misimu miwili mara baada ya kuondoka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Southampton katika uwanja wa Wembley jioni ya leo.

Chelsea ilianza kipindi cha kwanza kwa kutengeneza nafasi nyingi za mashambulizi uku Willian akiishia kugongesha mwamba katika shambulizi lililotengenezwa vyema na Eden Hazard. Mashambulizi mengi yalitengenezwa lakini bado bahati haikuwa upande wa Chelsea na hatimaye kipindi cha kwanza kikamalizika kwa matokeo ya sare ya  0-0.

Kipindi cha pili kilianza na Chelsea ikatengeneza shambulizi moja hatari, shukrani kwa Eden Hazard aliyetumia umahiri wake mkubwa kuumiliki mpira na kutoa pasi kwa Olivier Giroud ambaye alifunga goli safi la ubora mkubwa akiwapiga chenga mabeki na kipa wao na kufunga goli safi lililoifanya Chelsea iongoze kwa goli moja. Goli hilo lilifungwa dakika ya 46. Baada ya mpira kuchezeka kwa muda, kocha Antonio Conte akafanya mabadiliko kumtoa Olivier Giroud na kumwingiza Alvaro Morata aliyeifungia Chelsea goli la pili akifunga goli kwa kichwa akipokea pasi safi kutoka kwa Cesar Azpilicueta.

Sasa Chelsea inafanikiwa kufudhu kucheza fainali ya kombe hilo la FA ambapo itacheza dhidi ya Manchester united ambao jana waliifunga Tottenham katika mchezo mwengine wa nusu fainali.

No comments:

Post a Comment