Habari muhimu kuelekea Chelsea vs Southampton, kombe la FA - Darajani 1905

Habari muhimu kuelekea Chelsea vs Southampton, kombe la FA

Share This

Chelsea inashuka uwanjani jioni ya leo kucheza mchezo wake wa nusu fainali ya kombe la FA dhidi ya Southampton katika uwanja wa Wembley uliopo jijini London nchini Uingereza.

Kuelekea kwenye mchezo huo, hapa nakuletea habari muhimu kuhusu mchezo huo ambao Chelsea inahitaji ipate ushindi ili kujiweka sawa kwenye mbio zake za kushinda taji msimu huu mara baada ya kupoteza mataji matatu iliyokuwa nayo kabla ya kuanza msimu ili kuyapigania kuyashinda.

Habari muhimu;
Chelsea: David Luiz, Danny Drinkwater na Ethan Ampadu bado wataendelea kuwa nje haswa kutokana na majeraha waliyoyapata. David Luiz anaweza akarejea mwishoni mwa msimu huu haswa kutokana na kuonekana anaimarika vyema na kuzidi kuwa sawa kiafya.

Southampton: Kocha Mark Hughes amesema hana mchezaji mpya aliyemajeruhi na amejiandaa vyema kucheza dhidi ya Chelsea katika nusu fainali hii.

Rekodi: Chelsea imefanikiwa kuvuka kucheza fainali mara 11 kati ya mara 14 ya kombe la FA.

Michezo iliyopita;
Chelsea: LLDWW
Southampton: WLLLD

Muda: Saa 05:00 Jioni (Saa 17:00) EAT

No comments:

Post a Comment