De Bruyne aeleza sababu ya kuondoka Chelsea - Darajani 1905

De Bruyne aeleza sababu ya kuondoka Chelsea

Share This

Kiungo wa klabu ya Manchester city ya nchini Uingereza, Kevin De Bruyne ambaye aliwai kuitumikia Chelsea kabla ya kuachana na klabu hiyo ambaye usajili wake wa kuondoka Chelsea unatajwa kufanyika kwa makosa ambapo kocha wa Chelsea aliyekuwa kipindi hicho amekuwa akilaumiwa kwa kumuuza mbelgiji huyo ambaye amekuwa bora kwenye klabu zote alizozichezea tangu aachane na Chelsea ambapo hakupata nafasi kubwa ya kuichezea klabu hiyo.

Wachambuzi wengi wa soka wamekuwa wakishangazwa na maamuzi ya kocha huyo ambaye pia alimuuza winga hatari raia wa Misri, Mohammed Salah ambaye kwa sasa ndiye mchezaji aliye kwenye ubora wa hali ya juu.

Mara baada ya lawama zote hizo kutolewa kwa kocha huyo ambaye amekuwa akishambuliwa kwa kushindwa kuwathamini wachezaji aliowai kufanya nao kazi kwenye klabu alizowai kupita, hatimaye Kevin De Bruyne mwenyewe ameeleza sababu haswa iliyomfanya akaachana na klabu ya Chelsea.

"Nafikiri kama kocha anataka kuongea nawewe basi nawe utafanya hivyo. Yeye ndiye 'boss'. Inatakiwa uwe na maelewano mazuri na kila mchezaji, lakini kwangu mi nayeye [Jose Mourinho] ilikuwa tofauti"

"Niliongea nae mara mbili tu, hiyo ndio sababu iliyonifanya nikaona ni bora niondoke, nilitaka nijiunge na Borrusia Dortmund mwanzoni mwa majira ya kiangazi. Nilihitaji kupata nafasi ya kucheza" alisema nyota huyo raia wa Ubelgiji.

Nyota huyo alisajiliwa na Chelsea mwaka 2012 akitokea klabu ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji, klabu inayochezewa na mtanzania, Mbwana Samatta ambapo alisajiliwa na Chelsea ikiwa chini ya kocha Di Matteo ambapo baada ya kusajiliwa alitolewa kwa mkopo na klabu ya Werder Bremen ambapo baadae mara baada ya kurejea Chelsea alikutana na kocha Jose Mourinho ambaye baadae alimuuza kwenda Wolfburg.

Nyota huyo atamenyana na kocha huyo raia wa Ureno mwisho wa wiki hii ambapo Manchester city itamenyana dhidi ya Manchester united huku akitajwa na wachambuzi wengi kama moja ya wachezaji bora ambao Chelsea ilikosea kuwauza.

No comments:

Post a Comment