Batshuayi afichua siri, kumbe alivunja sheria akiwa Chelsea - Darajani 1905

Batshuayi afichua siri, kumbe alivunja sheria akiwa Chelsea

Share This

Nyota wa Chelsea, Michy Batshuayi anayeichezea kwa mkopo klabu ya Borrusia Dortmund amekuwa na msimu mzuri tangu ajiunge na klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu nchini Ujerumani maarufu kama Bundesliga alifanyiwa mahojiano na kuulizwa maswali mengi na ubora aliokuwa nao tangu ajiunge na klabu hiyo katika dirisha la usajili la mwezi Januari ambapo mpaka sasa ameshafunga magoli nane katika michezo 11.

Lakini katika maswali mengi aliyoulizwa katika majibu yake alitoa jibu mojawapo akieleza juu ya kuwai kuvunja sheria ya mkataba wake na klabu ya Chelsea pindi alipokuwa klabuni huko.

"Mikataba mingi ya wachezaji wa soka inakataza juu ya kucheza mchezo wa Futsal, lakini mi niliucheza kwa siri. Hakuna aliyejua mpaka leo" alisema mbelgiji huyo ambae kwa sasa ana miaka 24 ambaye alikiri kuucheza mchezo huo pindi alipokuwa akikosa nafasi kwenye kikosi cha Chelsea.

Futsal ni mchezo wa soka ambao unachezwa kama mpira wa miguu wa kawaida ila tofauti yake na mpira wa miguu ni kwamba Futsal unachezwa kwenye uwanja wenye kibaraza tofauti na huu mwengine ambao unachezwa kwenye uwanja wa nyasi lakini pia Futsal unachezwa na timu mbili zenye wachezaji watano kila upande wakati soka ni wachezaji kumi na moja kila upande.

Sababu ya mikataba ya wachezaji kukatazwa kuucheza mchezo huu na mingine ni kutokana na uhatari wa michezo hiyo kuweza kumsababisha mchezaji akapata majeraha haswa kwa Futsal ambao ni lazima uwanja wake kuwa wa kibaraza basi inaweza ikampa mchezaji majeraha ya muda mrefu

No comments:

Post a Comment