Chelsea inaamka kutoka usingizi mara baada ya kuwa nyuma kwa magoli mawili kabla ya kusawazisha na kupata ushindi mnono unaoifanya Chelsea kurudisha matumaini yake ya kufudhu kucheza klabu bingwa barani Ulaya kwa msimu ujao.
Kiukweli kila shabiki wa Chelsea alikuwa kwenye huzuni kwenye dakika 69 za mchezo huo ambapo dakika 45 za kipindi cha kwanza zikiisha kwa Chelsea ikiwa nyuma kwa goli 1-0, goli lililomfanya kila shabiki wa Chelsea kuona huu sasa ni mwaka wa shetani.
Kipindi cha pili kilianza huku Chelsea ikiendeleza ubovu wake haswa kwenye safu ya ushambuliaji ambapo ilitengeneza nafasi nyingi za kusawazisha lakini kutokuelewana kwa safu ya ushambuliaji kunaonekana kuitafuna sana klabu yetu. Dakika kadhaa baadae Southampton wakapata goli la pili mara baada ya kiungo wa Chelsea, N'Golo Kante kumchezea madhambi mchezaji wa wapinzani wetu hao na ndipo wakazawadiwa mpira wa adhabu na wakautumia vizuri na kuifanya Chelsea kuruhusu goli la pili.
Sasa utamu wa siku ulianzia pale kocha Antonio Conte alipofanya mabadiliko yake ya kumwingiza Olivier Giroud pamoja na Pedro ambao walichukua nafasi za Alvaro Morata na Davide Zappacosta.
Shambulizi likatengenezwa, Marcos Alonso kwa kutumia miguu yake mizuri yenye ufundi mkubwa ya kuwatesa makipa wa timu pinzani akapiga krosi nzuri na tamu iliyomkuta Olivier Giroud kisawasawa na kuifanya Chelsea kusawazisha goli kabla ya dakika kadhaa tena Eden Hazard kukata ukame wa kuhusika kwenye ufungaji kwa kufunga goli jengine lenye utamu mwingi mwingi.
Wakati matokeo yakiwa 2-2 ndipo Olivier Giroud akaongeza tena kwa goli lake la tatu lililoipa Chelsea ushindi wake muhimu na kuifanya Chelsea kuondoka na ushindi muhimu wa magoli 2-3 na kuifanya Chelsea kufikisha alama 60 huku tukiachwa alama saba na Tottenham yenye alama 67.
Mchezo unaofata;
Burnley vs Chelsea
Siku: tarehe 19-Aprili
Uwanja: Turf Moor
No comments:
Post a Comment