Habari muhimu kuelekea Newcastle vs Chelsea - Darajani 1905

Habari muhimu kuelekea Newcastle vs Chelsea

Share This

Leo ni siku ya mwisho kwa ligi kuu Uingereza ambapo Chelsea inashuka uwanjani ikiwa ugenini ili kucheza mchezo wake wa raundi ya 38 dhidi ya Newcastle united inayofundishwa na kocha wa zamani wa Chelsea, Rafa Benitez ambaye aliwai kuisaidia Chelsea kushinda taji la ligi la barani Ulaya (Europa League) mwaka 2013.

Kuelekea kwenye mchezo huo hapa nakuletea habari muhimu juu ya mchezo huo ambao Chelsea inabidi ipate ushindi ili kutetea nafasi ya kufudhu kucheza klabu bingwa barani Ulaya lakini lazima Liverpool ipoteze kwenye mchezo wake dhidi ya Brighton & Hove.

Habari muhimu;
Chelsea; Kocha Antonio Conte alisema mlinda mlango nambari moja,  Thibaut Courtois yupo sawa kiafya licha ya kukosa mchezo uliopita wakati Chelsea ilipomenyana dhidi ya Huddersfield ambapo nafasi ya mlinda mlango huyo ilichukuliwa na Willy Caballero ambaye ni mlinda mlango nambari mbili.

Nyota watakaoukosa mchezo huu kutokana na majeraha ni pamoja na Ethan Ampadu pamoja na mbrazili, David Luiz.

Newcastle; Robert Kenedy ataukosa mchezo huu kutokana na sheria ya ligi kuu kutoruhusu mchezaji aliye kwa mkopo kucheza dhidi ya timu yake na winga huyu yupo kwa mkopo klabuni hapa huku akiwa ni mchezaji wa Chelsea. Islam Slimani nae anaukosa mchezo wa leo mara baada ya kupewa adhabu ya kuikosa michezo mitatu na sasa amerejea klabuni Leicester city, klabu iliyompeleka kwa mkopo klabuni Newcastle.

Mwamuzi; Martin Atkinson atakuwa mwamuzi wa mchezo wa leo ambapo mara ya mwisho kuchezesha mchezo wakati Chelsea ikiwa uwanjani ilikuwa kwenye mchezo wa nusu fainali ya kombe la FA dhidi Southampton pale kwenye uwanja wa Wembley.

Rekodi; Katika michezo ya mwisho ya ligi kuu Uingereza, Chelsea ndio klabu iliyopata ushindi mnono wa magoli 8-0 dhidi ya Wigan Athletic ambapo ilitwaa taji hilo la ligi kuu Uingereza kwa msimu wa 2009-2010.

Michezo iliyopita;
Chelsea: DWWWD
Newcastle: WLLLL

Muda: Saa 05:00 Jioni (Saa 17:00) kwa saa za Afrika Mashariki (EAT)

No comments:

Post a Comment