Klabu ya soka ya wanawake ya Chelsea maarufu kama Chelsea Ladies imefanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Sunderland kwenye mchezo wake wa nyumbani, Kingsmeadow katika ligi kuu nchini Uingereza kwa wanawake (FA WSL).
Chelsea ilifanikiwa kupata ushindi huo ambapo magoli yaje yalifungwa na mshambuliaji wake hatari, Fran Kirby ambaye alifunga goli hilo katika kipindi cha kwanza wakati kipindi cha pili goli lilifungwa na Enia Aluko ambaye aliifungia goli hilo likiwa ni goli lake la 67 tangu afike klabuni Chelsea.
Lakini kabla ya mchezo huo kuanza kulitolewa zawadi za aina mbili ambapo zawadi ya kwanza ilitolewa kwa nahodha wa klabu hiyo, Katie Chapman ambae alikuwa akiichezea Chelsea mchezo wa 100 huku akiwa tayari ameshatangaza kuachana na uchezaji wa soka kwa sasa akiwa na miaka 35 lakini pia ukiwa mchezo wa mwisho kuucheza akiwa nyumbani Kingsmeadow ambapo kwa sasa imebakiza michezo miwili ya ligi kuu ili ligi hiyo iishe.
Zawadi nyengine ni pamoja na tunzo maalumu iliyotolewa na kundi la mashabiki wa klabu hiyo ya wanawake ambapo waliungana na kuona Fran Kirby kuwa mshindi wa tunzo hiyo ya mwaka.
Kwa matokeo haya, Chelsea Ladies inahitaji ipate alama moja ili iweze kuwa mabingwa wa ligi kuu huku ikibakiza michezo miwili mpaka sasa.
No comments:
Post a Comment