Chelsea imeshindwa kupambania nafasi yake ya kushiriki michuano ya klabu bingwa barani Ulaya kwa msimu ujao mara baada ya kupoteza kwa magoli 3-0 dhidi ya Newcastle United kwenye mchezo wa mwisho wa ligi kuu Uingereza uliomalizika kwa Manchester city kutwaa taji la ligi kuu nchini humo na mpaka sasa Chelsea imebakiza nafasi ya taji moja tu kulibeba msimu huu, taji la kombe la FA ambapo hiyo bado haionekani kumfanya kocha Antonio Conte kuendelea kusalia kuwa kocha wa klabu hiyo.
Mengi yameongelewa na bado yanazidi kuongelewa juu ya nafasi ya kocha huyo kuendelea kuifundisha Chelsea ambapo kati ya hayo mengi kubwa zaidi linaloongelewa ni kocha huyo kutimuliwa klabuni hapo licha ya kubakiza mkataba wa mwaka mmoja.
Moja ya nyota waliowai kuchezea klabuni Chelsea, Steve Sidwell amefanyiwa mahojiano na kuulizwa nafasi ya kocha huyo kusalia Chelsea huku kocha anayetajwa kuwaniwa na klabu hiyo, Mauricio Pochettino bado zikiwa zimekolea.
"Hakuna moshi mahali ambapo hakuna moto, naamini kuna ukweli juu ya hili (la Pochettino kumrithi Antonio Conte) na ukiangalia kwa upande wake (Pochettino) anahitaji mkataba mpya huenda pia hii ikawa ni akili ya kibiashara inayofanywa na wakala wake ili apate faida kubwa"
"Lakini kama taarifa hizo ni za kweli basi namkaribisha kwa mikono miwili. Amekua ni kocha bora tangu amefika Uingereza, aliyoyafanya akiwa na Southampton hakika lilikua ni jambo kubwa"
"Napenda jinsi anavyofanya kazi na klabu yake, na ukiangalia fungu analolitumia na makubwa aliyoyafanya kila mtu ambaye amefanya kazi chini yake amekua akisifia juu ya ufundishaji wake na kiasi gani alivyokua bora"
"Na ukiangalia kwenye klabu alizozipitia Southampton na Tottenham naamini hata wale wachezaji vijana pale Chelsea watatamani atue pale" alisema nyota huyo
Mauricio Pochettino ambaye ni kocha wa Tottenham amekua akitajwa kwa karibu kutakiwa na Chelsea.
No comments:
Post a Comment