Moja ya chombo cha habari kiliripoti biashara ya Chelsea kumnasa kocha wa zamani wa Napoli, Maurizio Sarri ingekamilika usiku wa ijumaa ya kuamkia leo jumamosi ambapo wawakilishi wa kocha huyo wangekutana ili kujadili juu ya mahitaji binafsi.
Na hatimaye biashara hiyo inaelezwa kuelekea kukamilika na kilichobaki kwa sasa ni kocha huyo kusaini mkataba wake wa miaka miwili aliokubaliana na Chelsea huku akipokea mshahara wa paundi milioni 5.25 kwa kila mwaka.
Taarifa hizo zilizotoka kama mwendelezo wa kocha huyo kutua Chelsea zinaeleza kuwa biashara hiyo inaweza ikakamilishwa na kocha huyo kutangazwa rasmi kama kocha wa Chelsea muda wowote kuanzia sasa huku mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich akimwachia majukumu yote kiongozi wa bodi ya usajili, Marina Glanovskaia.
Lakini Chelsea haitokua na kazi rahisi juu ya biashara hii ambapo itahitaji kiasi cha paundi milioni 8 ili kuilipa Napoli kama ada ya kocha huyo kuondoka klabuni hapo haswa kutokana na bado alikua na mkataba wa mwaka mmoja klabuni hapo kwa maana hiyo bado anahesabika wa Napoli licha ya klabu hiyo kumteua Carlo Ancelotti kama kocha wake mpya.
Ila pia Chelsea itatakiwa kuandaa paundi milioni 9 kama dau la fidia kwa kocha Antonio Conte ambaye alibakiza mkataba wa mwaka mmoja ambao kama angeumalizia basi angeondoka Chelsea kama mtu huru ila kuondoka kwake tena kwa Chelsea kuvunja mkataba wake hii itailazimu Chelsea imlipe kocha huyo mshahara wake ambao angetakiwa alipwe kama angeendelea kusalia klabuni hapo.
No comments:
Post a Comment