Messi apagawa na ubora wa nyota wa Chelsea, awaagiza Barcelona kumsajili - Darajani 1905

Messi apagawa na ubora wa nyota wa Chelsea, awaagiza Barcelona kumsajili

Share This

Nyota wa klabu ya Barcelona ya nchini Hispania, Lionel Messi ambaye ataiongoza timu yake ya taifa ya Argentina kwenye michuano ya kombe la dunia kwa mwaka huu wa 2018 huko nchini Urusi ametoa angalizo kwa klabu yake kama itataka kufanya vizuri na kufikia mafanikio makubwa basi ihakikishe inamnasa mlinzi na winga wa kushoto wa Chelsea, Marcos Alonso.

Messi anatajwa kuishawishi klabu yake imsajili Marcos Alonso ili ijiweke sawa kuelekea msimu ujao ambao Barcelona atakuwa bingwa mtetezi wa mataji mawili ambayo ni la ligi kuu Hispania pamoja na kombe la mfalme maarufu kama Copa del Ley.

Marcos Alonso ameendeleza msimu wake bora akifunga magoli nane kwa msimu huu kwenye mashindano yote na kumfanya kuchaguliwa kwa mara ya kwanza kuichezea timu yake ya taifa ya Hispania uku akichaguliwa pia kuingia kwenye kikosi bora cha ligi kuu Uingereza kilichotolewa na chama cha wanasoka wakulipwa (PFA).

Dau linakisiwa kuigharimu Barcelona ili imnase nyota huyo ni paundi milioni 35.

No comments:

Post a Comment