Hazard na Conte kumekucha, amuongelea Maurizio Sarri - Darajani 1905

Hazard na Conte kumekucha, amuongelea Maurizio Sarri

Share This

Nyota wa Chelsea, Eden Hazard ambaye wiki iliyopita siku kams ya leo aliiongoza Chelsea kushinda taji lake pekee kwa msimu huu akiibamiza Man utd goli moja la pekee kwenye mchezo huo na kuifanya Chelsea iliyochini ya kocha Antonio Conte kushinda taji lake la pili ndani ya misimu miwili, lakini nyota huyo anatajwa kushinikiza kuondoka kwa kocha wa sasa Antonio Conte na kuletwa kocha Maurizio Sarri ambaye amekua akitajwa kwa karibu kutua Chelsea.

Nyota huyo raia wa Ubelgiji anatajwa kuvutiwa na sifa za kocha huyo aliyeifundisha klabu ya Napoli kwa msimu uliopita ambapo sifa za kocha huyo anezipata kwa nyota mwenzake wa Ubelgiji, Dries Mertens ambaye amefundishwa na kocha huyo klabuni Napoli kabla ya kukataa kusaini mkataba  mpya wa kuendelea kuifundisha Napoli kwa msimu mwengine na tayari nafasi yake imeshachukuliwa na Carlo Ancelotti.

Habari na ripoti zinadai Hazard amepewa sifa nyingi kumhusu kocha huyo mwenye miaka 59 hali iliyomfanya kutamani kufundishwa na kocha huyo ambaye kwenye maisha yake ya soka ya kuwa kocha kwa miaka 13 ila ameshindwa kutwaa taji lolote.

Taarifa zilizopo ni kwamba Chelsea imefikia makubaliano na kocha huyo ambapo anaweza akatua Chelsea kwa mkataba wa miaka miwili huku ikidaiwa anaushawishi uongozi wa klabu hiyo ya jijini London kukamilisha usajili wa nyota wanne kutoka Napoli ili aweze kutua nao Chelsea. Kama unataka kuwasoma nyota hao, bonyeza hapa

No comments:

Post a Comment