Chelsea yakamilisha msimu kwa ubingwa mwengine - Darajani 1905

Chelsea yakamilisha msimu kwa ubingwa mwengine

Share This

Walianza vijana wa Chelsea wenye umri chini ya miaka 18 ambao walikuwa na msimu mzuri zaidi kwa kubeba mataji manne kwa msimu huu wakafata kikosi cha wanawake wa Chelsea waliobadili jina kwa sasa na kuitwa Chelsea FC Women kutoka Chelsea Ladies ambao wao wametwaa mataji mawili ambayo ni ya ligi kuu Uingereza pamoja na kombe la FA kwa wanawake ambapo waliibamiza Arsenal kwa mabao 3-1 wakafata tena kikosi chenyewe cha vidume wa Chelsea ambao waliitumbukiza Man utd katika fainali ya kombe la FA kwenye uwanja wa Wembley na kufanikiwa kushinda taji hilo pekee msimu huu.

Na sasa ni zamu tena ya vijana wa Chelsea ambao hawa ni wale wenye umri chini ya miaka 15 ambao wameshinda taji la tatu msimu huu wakiibamiza klabu ya vijana wenzao wa Aston Villa kwa mabao 3-1 na kufanikiwa kutwaa taji hilo la Premier Floodlit.

Magoli matatu ya vijana hao wa Chelsea yalifungwa Joe Haigh, Sam Iling pamoja na Nathan Young-Coombes.

Hongereni vijana...

No comments:

Post a Comment